Advertisement

MILIKI2

JE UNASUMBULIWA NA WEUSI WA KWAPA?

 Weusi chini ya kwapa sio ugonjwa ni mabadiliko ya ngozi unapata watu wengi na kuwafanya wasiwe comfortable kuvaa nguo za wazi mbele za watu. Hali ya kuwa mweusi kwapani hutokana na kufa kwa baadhi ya cell, kutumia dawa ya kunyolea na kupaka deudorant yenye alcohol


Kuna njia za kawaida ambazo zitaweza kusaidia kuondoa weusi katika makwapa yako na kukufanya urejee katika muonekano wako zamani.

a.)Limao:- Chukua limao au ndimu kata vipande duara upake sukari au asali kwa juu ,kisha chukua hivyo vipande ujipake makwapani mara 2 kwa siku acha kwa dakika 10 kabla hujaenda kuoga kisha osha kwa maji vugu vugu.

b.)Baking soda:-inasaidia kutoa cells zilizokufa kwa urahisi ,changanya baking soda na maji iwe nzito nzito paka kwapani acha kwa dk 10 osha na jikaushe fanya hivyo mara 2-3 kwa wiki. Endela na zoezi hilo mpaka utakapo ridhika na mabadiriko uliopata.


c.)Tango:- Tumia vipande na ujipake kwapani yale maji yake ndio dawa au saga iwe nyepesi na upake ikae kwa dakika 10-20 kwapani .

d.)Sukari:- Tumia brown sugar changanya na olive oil paka badaa ya muda wa dakika 10 osha.


e.)Mafuta ya nazi- ni tiba nzurisana na yamekuwa na mchango wa kutosha kwani yana vitamini E yanasaidia kung’arisha ngozi, chukua mafuta ya nazi paka kwapani baada ya dk 10-20 toa na kunawa kwa maji ya vuguvugu .


Zoezi la kuondoa weusi kwapani linaweza kuchukua muda ila hakikisha unafuata maelekezo kwani yatakupa matokeo mazuri sana🥰🥰🥰

Post a Comment

0 Comments