Advertisement

MILIKI2

NJIA RAHISI KABISA ZA KUONDOA CHUNUSI BILA GHARAMA KUBWA

JINSI YA KUONDOA CHUNUSI( ni nzuri zaidi kufanya wakati wa usiku)

Wakati watu wengi wakitumia mafuta pia na lotion zenye viambatana sumu yani kemikali na kuharibu ngozi zao za uso (reception) but Kuna njia za asili na za kuaminika za kuondoa chunusi na hazihitaji pesa nyingi kutumia

1.Kipande cha barafu 
Barafu husaidia kukausha/kunyausha chunusi  na kunyonya mafuta na kuyasambaza katika maeneo mengi ya mwili

Namna ya kutumia
Chukua barafu tia kwenye kitamba safi then fanya kama una massage sehemu yenye chunusi
Fanya mara nyingi uwezavyo

2.Asali
Pia imethibitishwa na wataalam wa ngozi kuwa asali inasaidiaa sana kuondoa chunusi kwa kuzibua matundu ya hewa ya ngozi na kufanya ngozi kupumua vizuri , endapo matundu yakizipa husababisha chunusi

Namna ya kutumia
Tumia pamba safi chovya asali paka katika eneo lenye chunusi fanya kama unamassage eneo, acha kwa dakika 10  osha kwa maji ya uvuguvugu

3.Maji ya limao (lemon juice)
Linauwa vijidudu katika ngozi pia huondoa chunusi haraka kwa sababu ya kemikali zipatikanazo ndani yake

Namna ya kutumia
 Tumia pamba safi weka kwenye eneo lenye chunusi  baadaa ya hapo lala mpaka asabuhi , nawa uso uamkapo

4.Dawa ya Meno
Dawa ya maajabu ya kuondoa chunusi haraka bila kuacha kovu, inakausha chunusi haraka sana

Namna ya kutumia
Chukua dawa kidogo weka eneo lenye chunusi mpaka asubuhi then nawa uso kwa maji safi

5.kitungu Swahumu
Kitungu hutibu magonjwa takribani 20 pia chunusi kwa uharaka sana

Namna ya kutumia
Kata kitungu swahumu vipande viwili
Sugua taratibu eneo lenye chunusi

6.chapa maandashi(baking powder)
Pia namna nyingine ya kuondoa chunusi, inasaidiaa kunyonya mafuta uso haraka sana na kuacha uso ukiwa mkavu na nyororo

Namna ya kutumia
-kijiko cha chai kimoja Cha chapa mandashi
-Maji kiasi au maji ya limao
-changanya
-Osha uso
-Paka mchanganyiko wako subili kwa dakika 5
-Osha uso kwa maji ya uvuguvugu
Kwa maswali TAFADHARI usisite kuuliza

Post a Comment

0 Comments