Advertisement

MILIKI2

TATIZO LA SAUTI KUKWARUZA AU KUPOTEA

Maelezo ya jumla



Tatizo la sauti kukwaruza au kupotea ni shida inayokera, sauti yako inakua inakwaruza kwaruza na inakuwa ngumu wewe kusikika unapoongea. Sababu ya kawaida huwa ni kuvimba kwa sanduku la kutengenezea sauti ‘’voice box’’ kwa sababu ya maambukizi kama vile mafua. Koo linaweza kuwa linawasha au kuuma na unaweza kuwa unahisi kama kuna uvimbe kooni. Unaweza kupoteza sauti ghafla kwa sababu ya matumizi mabaya ya sauti – kwa mfano kama unaongea kwa nguvu sana au unashangilia kwa nguvu sana wakati wa mechi ya mpira wa miguu. Ukiona tatizo la kukwaruza kwaruza sauti linaanza taratibu linaweza kuwa limesababishwa na matumizi mabaya ya sauti, kuvuta sigara au kucheua kwa asidi ya tumbo ambayo pia inasababisha kiungulia na kusumbua sanduku la kutengenezea sauti kooni. Kwa kesi chache tu, kukwaruza kwaruza kwa sauti kunaweza kuwa dalili ya mwanzo ya kansa ya koo.

Unachoweza kufanya mwenyewe ukiwa na tatizo la sauti kukwaruza au kupotea

Kwa kawaida tatizo la kukwaruza au kupotea kwa sauti huwa ni la muda na huwa halidumu zaidi ya wiki moja. Ukifuata njia zifuatazo itasaidia kurudi haraka kwa sauti yako

  • Pumzisha sauti kadri inavyowezekana. Usiongee au kunong’oneza. Kunong’oneza kunaweza kusababisha misuli ya koo kukaza zaidi kuliko hatanukiongea kawaida.
  • Kunywa maji ya kutosha ili kupooza koo, kunywa angalau glass 6-8 za maji ili kuepuka koo kukauka sana. Usinye vinywaji vyenye caffeine kama vile kahawa, cola, chai au pombe
  • Kula vyakula laini ambavyo vitakuwa rahisi kumeza
  • Epuka kukaa maeneo yaliyo makavu sana au yenye moshi mwingi ambao unaweza kukausha zaidi koo na kusababisha hali ya sauti kuwa mbaya zaidi
  • Kama koo linauma sana, tumia dawa za kupunguza maumivu, madawa kama vile ‘’acetaminophen’’ yatasaidia kupunguza maumivu ya koo na kukwaruza kwaruza kwa sauti
  • Unaweza pia kujifukiza ili kupunguza kuvimba kwa koo na kuongeza unyevu kooni. Weka maji ya moto kwenye bakuli na kisha chukua kitambaa jifunike kichwani ukiwa umeinamia maji hayo ya moto (yasiwe yanachemka yakakuunguza). Vuta pumzi kupitia pumzi zako ili kuruhusu mvuke uingie
  • Usi-gogomoe ‘’gargling’’ – haisaidii, madawa ya kikohozi pia hayasaidii kurudi kwa sauti pia

Tatizo la sauti kukwaruza au kupoteaKugogomoa

Mwone daktari kama:

  • Kama sauti yako bado inakwaruza kwa zaidi ya wiki 2 hata baada ya kufuata ushauri ulio hapo juu
  • Kama sauti yako inakwaruza au imesha na unapata shida ya kupumua au unapata shida kumeza

Post a Comment

0 Comments