Advertisement

MILIKI2

JE NYWELE ZAKO HAZIKUI NA ZIMEDUMAA?

 JINSI YA KUKUZA NA KUJAZA NYWELE ZILIZODUMAA


Tumia tiba asilia kukuza/kujaza nywele zako.

Zifuatazo ni tiba mbalimbali zinazoweza kukusaidia kujaza na kukuza nywele zako.

Angalia aina mojawapo ya tiba ambayo ni rahisi kwako Kisha itumie ...itakusaidia


1)Kitunguu maji (Onion)

Kata vipande vidogovidogo vya vitunguu maji weka kwenye shampuu yako acha vikae kwa muda wa siku 15 kisha tumia shampoo yako, si kwamba itasaidia kukuza nywele zako tu bali itasaidia kuzifanya nywele zako zingae na ziwe na afya.


 

2)Mdarasini, Kitunguu maji chekundu,karafuu na kitunguu swaumu





Kata kitunguu maji chekundu nusu changanya na karafuu tatu, kitunguu swaumu na miti miwili ya mdarasini. Weka kila kitu kwenye sufuria chemsha kwa muda wa dakika 15. Ukishafanya hivyo acha mchanganyiko wako upoe kisha uoshe nywele zako kila siku kwa siku nne.


 

3)Mafuta mbegu za zabibu ‘Grape seed oil’m


Mafuta ya zabibu yanaaminika kwenye kukuza nywele, tumia mafuta hayo kupaka kwenye ngozi chini ya nywele kisha fanya masaji kabla ya kupana kitanda.


4)Aloe Vera na asali (honey)


Kata majani matatu ya aloe vera toa ute wake changanya na asali kisha paka chini ya ngozi acha kwa muda wa dakika 20 kisha safisha.


 

5)Maji ya rozi (Rosemary water)

kila siku pakaa maji ya rozi kwenye nywele zako hasa eneo la chini ya ngozi.


6)Maji ya viazi (Potato water )

Kama utakuwa unapika viazi chukua maji ya viazi yaliyopata moto osha nywele zako, yanasaidia kukuza nywele.

Post a Comment

0 Comments