Advertisement

MILIKI2

JE UNAPENDA UREMBO WA KOPE NDEFU?

 JINSI YA KUJAZA NA KUREFUSHA KOPE ZAKO

 Leo nimekuja na urembo unaotesa wanawake wengi mpaka wanahangaika kuweka za kununua,Kope ni moja ya kivutio katika uso,ndio maana watu wanahangaika kuweka za bandia.Kitu kibaya kwenye kope za bandia ukiweka muda mrefu unapoteza hata zile chache ulizokuwa nazo mwanzoni.Hii sio tu kwa wanaotaka kujaza kope bali hata wale ambao kope zao zimeharibiwa na matumizi ya kope bandia.


MAAJABU YA VASELINE KATIKA KUKUZA NA KUJAZA KOPE

Naiongelea ile Vaseline blue seal ambayo wengi tunatumia kupaka kwenye ngozi.Kwenye kukuza na kujaza kope paka Vaseline kwenye kope zako kila siku jioni kabla ya kulala.Baada ya wiki mbili hadi tatu utaona mabadiliko.



Post a Comment

0 Comments