Advertisement

MILIKI2

JINSI YA KUWA NA MIGUU LAINI YENYE KUNG'AA

 Je wasumbuliwa na miguu mikavu na NGOZI ngumu ya miguuni hasa unyayo?



Leo tutaangalia jinsi au namna gani ya kupata ngozi nzuri ya miguu bila ya kwenda kusuguliwa saluni kama wafanyavyo wanawake wengi.

  Urembo huu rahisi,tena kwa gharama nafuu unaweza kuupata nyumbani kwako tu na ukaonekana mwenye mvuto zaidi,je? utafanyaje soma hapa:

LIMAO ,ASALI NA MAFUTA YA MZAITUNI

>>Limao ukichanganya na asali pamoja na mafuta ya mzaituni au ukichukua limao ukachovya kwenye asali na mafuta ya mzaituni kisha ukasugua miguu yako Kwa muda wa dakika 7-10,utapata majibu mazuri.

Baada ya kuisugua acha kwa muda wa dakika 10-20 kisha paka mafuta au losheni unayoitumia.


MAZIWA MGANDO

Maziwa mgando ni mazuri kwa kuondoa sugu kwenye miguu cha kufanya chukua maziwa hayo paka kwenye miguu yako acha kwa muda wa dakika 10-15 kabla ya kuosha,fanya hivyo kila unapokuwa na nafasi utaona jinsi utakavyo kuwa na ngozi laini isiyokuwa na sugu wala haina haja ya kwenda kuoshwa sehemu.


MAFUTA YA NAZI

Chukua mafuta ya nazi paka eneo lililopasuka taratibu fanyia masaji usiku,

Kazi ya mafuta ya nazi ni kulainisha ngozi yako na kuifanya ilainike,ukifanya hivyo utasahau kabisa kwenda kuosha miguu saluni.

Unaweza chagua Njia Moja ya kutumia na ukawa waifanya mara Kwa mara.

Post a Comment

0 Comments