Advertisement

MILIKI2

ONDOA MADOA USONI KWA KUTUMIA LIMAO NA ASALI TU.



Kumekuwa na sababu mbalimbali zinazofanya watu kutokuwa na ngozi zisizokubalika.Mbali na hali ya hewa pia matumizi ya pombe na sigara hata matumizi ya cream kali ambazo zimekuwa zikitumiwa na watu bila kujua madhara yake kumechangia kwa kiasi kikubwa tatizo hilo.

Ulaji wa matunda na mboga za majani kwa wingi kunywa glasi nane za maji kwa siku ni njia nzuri kama unataka kuwa na ngozi nzuri isiyo na madoa wala ukavu ambao haupendezi.

Wengi wanaacha kula mbogamboga na matunda kwa wingi hata kutokunywa maji ya kutosha na badala yake wamekuwa akitegemea kuwa na ngozi nzuri jambo ambalo ni gumu.
Mara kadhaa tumeshuhudia watu wanaopaka cream kali wakiwa kama wameungua usoni huku uso na mwili ukionekana kuwa makavu jambo ambalo linaashiria kuwa kupaka cream si suluhisho pekee la kuwa na ngozi nzuri.

Kuna watu wamekuwa na ngozi za asili na hata unapowauliza baadhi yao hawajawahi kupaka cream hata siku moja na bado wana ngozi nzuri zinazovutia hao wamekuwa wakila kwa ajili ya kuhakikisha wanatengeneza ngozi zao kutoka ndani.

Pia wengi wanaharibu ngozi zao na kuwa na madoa kutokana na kutumia make up kwa muda mrefu na hata anapogundua kuwa ana tatizo la madoa amekuwa akijaribu kutumia cream nyingine kwa ajili ya kumaliza tatizo hilo jambo ambali linazidisha madhara kwenye ngozi.
Unaweza kutibu ngozi yenye madoa usoni pia mashavuni kwa kujitibu na

  • juisi ya limao

Namna ya kufanya

  • Chukua limao lioshe na kisha likamue na kuchuja mbegu zake Kisha changanya kwenye asali mbichi. Weka juisi hiyo kwenye kikombe na kisha tafuta kitambaa laini kichovye kwenye mchanganyiko huo Kisha paka kwenye sehemu zenye tatizo.Kaa kama dakika tano kisha osha uso wako kwa maji safi.
Pia waweza TUMIA LIMAO KUONDOA WEUSI KWENYE KWAPA 
  • Limao lina sifa kubwa ya kuzuia harufu pia unaweza kulitumia katika kuondoa harufu kali ya jasho mwilini na husaidia kuondoa weusi kwenye kwapa, chini ya macho na mapajani pia  ........
Jinsi ya kufanya
  • Chukua kipande cha limao weka sukari kidogo, sugua. Unatakiwa kutumia kwenye kwapa ambalo ni safi, vizuri kutumia njia hii kabla na baada ya kuoga

Post a Comment

0 Comments