Advertisement

MILIKI2

NAMNA YA KUPATA RANGI MOJA MWILINI KWA KUTUMIA VITU VYA ASILI

 

Namna Ya Kupata Rangi Moja Mwilini Kwa Kutumia Vitu Vya Asili

Home remedy hii asili yake ni Jamaica. Kama wataka ngozi ya mwili yenye rangi moja, hii ni kwa ajili yako. 


Mahitaji

  • Vijiko 3 vya mafuta ya nazi ya uvuguvugu
  •  Juisi ya zabibu nusu
  • Kikombe kimoja cha sukari ya brown Muda wa kuandaa : Dakika 2


Maelekezo. 

1. Weka mahitaji yote kwenye bakuli kubwa na safi 

2. Changanya vizuri 

3. Ukiwa unaoga, paka scrub yako mwilini tu na usugue taratibu kwa kuzunguka eneo husika.

4. Osha 


Hii inaondoa Weusi Weusi katika maeneo ya mwili. Kati Kati ya mapaja Weusi kwenye kwapa Na Kama unapenda uwe na rangi moja mwilini. 


Tumia Kwa wiki Mara 2.


Kwa nini inafanya kazi. 

  • Zabibu zina anti oxidant inalinda ngozi kupata free radicals na hivyo inaondoa madoa meusi. 
  • Mafuta ya Nazi yanafaa kwa ngozi kukupa mng’ao na Ngozi nyororo. Yana virutubisho muhimu Ambazo zinanawirisha ngozi. 
  • Sukari ya Brown ni laini ukilinganisha na chumvi. Vipande vidogo vidogo vilivyopo vina Ondoa ngozi iliyokufa na kukuacha na mng’ao asili. Baada ya kutumia hii ule mng’ao wako wote utarudi katika nafasi Yake. 
  • Fanya Mara mbili kwa wiki hadi uone matokeo. 

Tahadhari

  • Usitumie usoni. Ngozi ya uso ni laini Sana ukilinganisha na mwilini hivyo mchanganyiko huu ni kwa ajili ya Ngozi yako ya mwili tu. 
  • Kama una rangi tofauti tofauti mwilini kwa sababu ya kujichubua na kutumia vipodozi vyenye kemikali na viambata sumu, utachelewa kuona matokeo zaidi kuwa mvumilivu!

Kama hujaanza kutumia, Anza Sasa! 

Mshirikishe na umpendae

Post a Comment

0 Comments