Advertisement

MILIKI2

KUZA NYWELE KWA MAJI YA MCHELE

 Ina shangaza ndio, na ina weza isiaminike lakini huo ndio ukweli. Maji ya mchele yana faida kubwa katika nywele una weza kuuliza kivipi na nani yame msaidia, ina semekana kabila la Yao kutoka kijiji cha Huangluo  Nchini China ndilo kabila ambalo lina wanawake wenye nywele ndefu zaidi duniani, ambapo wanaweza kufunga nywele zao kama kiremba


Wanawake hawa wanaamini kutumia maji ya mchele kuoshea nywele zao ndiko kunako fanya nywele zao kuwa ndefu zenye afya na kuto kupatwa kwa mvi mpaka katika miaka ya 80, huko china una weza kununua maji haya ya mchele na pia kuna site mbali mbali duniani wanayauza kwa $23 sawa na Tsh26933 lakini pia unaweza kufanya mwenyewe


Unacho takiwa kufanya ni wakati una pika mchele wako (wali) ongeza maji kidogo tofauti na yale uliyo yazoea kisha yakisha chemka na kuanza kuwa mazito na kubadilika rangi kuwa ya mchele punguza kwenye kibakuli na uyaache ya poe, baada ya hapo yakisha poa paka kwenye nywele zako na ukae nayo kwa muda wa dakika 3-5 na uoshe kwa maji masafi.


husaidia kukuza, kulinda nywele zisikatike na zilizo katika kurudi katika hali yake ya kawaida pamoja na ku ng’arisha nywele.

Post a Comment

0 Comments