Siku moja nilisimama mbele ya kioo kwa zaidi ya dakika tano, nikiangalia nywele zangu.
Nikavuta pumzi ndefu…😔
nikasema kimoyomoyo,
“Leo tena nifanye nini?”
Nilikuwa nimechoka.
Kukaa salon muda mrefu.💆
Kuvuta nywele mpaka kichwa kinauma.
Kutumia bidhaa nyingi bila kuona mabadiliko.🙎
Lakini zaidi ya yote —
nilikuwa nimechoka kujihisi si mzuri kwa sababu ya nywele zangu.😥
Sikujua nifanye Nini😩
Siku hiyo sikutaka drama.
Sikutaka stress.
Nilitaka kitu chepesi.
Nikaamua liwalo na liwe🙎
Nikagawanya nywele zangu mara mbili.
Nusu ya juu nikaisuka taratibu,
nusu ya chini nikaiweka kwa urahisi.
Hakukuwa na maumivu.
Hakukuwa na kukaa chini muda mrefu.
Hakukuwa na kuvuta mizizi.
Nilipojimaliza, nikajiangalia tena kwenye kioo.
Nikacheka kidogo.🥰😊
Kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu…
nilijisikia mzuri.😍
Na hapo ndipo niligundua kitu kikubwa sana:
👉 Uzuri hauhitaji mateso.
👉 Urembo hauhitaji haraka.
👉 Nywele zako hazihitaji kupigana nawe — zinahitaji upendo.
Style hii ilinifundisha zaidi ya kusuka.
Nilijifunza kuwa unaweza kuslay bila kuumiza nywele zako.
Nilijifunza kuwa unaweza kuwa classy hata kwa style rahisi.
Nilijifunza kuwa nywele natural — hata kama ni fupi — zina thamani.
Kwa sababu mtindo huu:
✔ hauna mambo mengi
✔ haumizi kichwa
✔ unaruhusu nywele kupumua
✔ unalinda ncha
✔ unachochea ukuaji wa nywele polepole
Lakini somo kubwa zaidi halikuwa kwenye nywele.
Lilikuwa moyoni.
Nilijifunza kuwa kila safari ya urembo inaanza na kujikubali.
Nilijifunza kuwa matokeo hayaji kwa haraka.
Nilijifunza kuwa kujipenda ni maamuzi ya kila siku.
Leo nikifanya style hii, simfikirii tena yule msichana aliyekuwa anaona nywele zake kama tatizo.
Namwona msichana aliyekuwa na ujasiri wa kuanza upya.
Kama na wewe umewahi kujisikia kuchoka na nywele zako…
nataka ujue hili:
Hauko peke yako.
Anza polepole.
Chagua styles protective.
Punguza stress.
Jipe muda.
Kwa sababu nywele hukua.
Urembo hujengwa.
Na wewe — unazidi kuwa mzuri kila siku na nywele zako ni sehemu ya uzuri wako❤️❤️❤️❤️
Tazama hapa namna ya kutengeneza mtindo huu RAHISI NDANI YA DAKIKA CHACHE 👇👇👇👇👇
Pia waweza pendelea kujifunza kusuka hatua kwa hatua👇 👇 👇 👇 👇
Usisahau ku'subscribe ili kuwa mwanafamilia wa Urembo na princes'Zey ❤️❤️❤️❤️




0 Comments