Na Princess Zey – Mtaalamu wa Urembo na Nywele
Nywele ni taji la kila mwanamke. Lakini ni mara ngapi umejiuliza kwa nini nywele zako haziongezeki urefu au hukatika kila mara? Jibu linaweza kuwa kwenye jambo rahisi sana – ncha zilizochoka.
Ncha Zilizochoka ni Nini?
Ncha zilizochoka ni sehemu za mwisho wa nywele ambazo zimechoka kutokana na kukosa unyevu, matumizi ya vifaa vya moto (kama pasi au blow-dry), au kutopata huduma sahihi kwa muda mrefu. Huwa kavu, nyepesi, hukatikakatika na hata hujikunja.
Kwa Nini Uziondoe?
Wengi huogopa kupunguza ncha kwa hofu ya “kupunguza urefu”. Lakini ukweli ni kwamba, kama huondoi ncha zilizokufa, zinaendelea kudhoofisha nywele nzima, na hata kukuzuia kufikia urefu unaotamani. Kwa kupunguza ncha:
Nywele hupumua na kuwa na afya zaidi
Hukua kwa kasi zaidi
Huonekana nadhifu, laini na zenye mng’ao
Ni Lini Upunguze?
Inashauriwa kupunguza ncha kila baada ya miezi 6 kwa nywele za kiafrika. Usihofu – huondoa tu sentimita 1 hadi 2, si urefu mzima!
Hitimisho
Kupunguza ncha si kupunguza urembo wako – ni kuutunza. Kama unataka nywele zako ziwe ndefu, zenye afya na mvuto wa asili, basi anza leo kwa kuchukua hatua hii ndogo lakini yenye nguvu kubwa.
Bonyeza hapa chini kutazama zaidi👇👇
Fuata @UrembonaPrincessZey kwa maarifa zaidi ya nywele, urembo wa asili na tutorials za kila wiki!
0 Comments