Advertisement

MILIKI2

NJIA 7 ZA KUPEWA HESHIMA POPOTE UENDAPO, UKIWA NA HALI YOYOTE

 Watu wengi wanaamini HESHIMA huletwa na pesa, cheo, elimu, umaarufu, mamlaka na nguvu kubwa ya ushawishi.....lakini wamesahau KUWA hivyo ni miongoni mwa vichochezi vya heshima tu bali heshima kamili unaweza kuipata kwa KUFANYA haya


MAMBO SABA YA KUZINGATIA ILI KUPATA HESHIMA

1) TAMBUA HAKI ZAKO

Ukiwa kazini, sokoni, barabarani, safarini au popote pale unapaswa kutambua HAKI zako.

Watu hukufanyia vitendo kutokana na vile unawaruhusu, ukikaa kimya MTU anapokuvunjia heshima ataendelea kukuvunjia heshima zaidi na zaidi.

Watu wanaokuvunjia heshima wakigundua unatambua haki zako watakuogopa zaidi na watakupa heshima zaidi.


2) WEKA MIPAKA

Ikiwa ni ndugu, rafiki, mfanyakazi mwenzako au jirani yako wawekee mipaka ya kukuzoea.

Acha kujishusha sana na Acha kujitoa sana, watu wengi hutafsiri huo kama udhaifu wako....na watakufanyia lolote kuvunja heshima yako


3) EPUKA KUONGEA WAKATI UNA HASIRA

Ikiwa una hasira ondoka eneo la ugomvi, hasira zikiisha mfate muhusika muelezee kwa utaratibu KUWA sijapenda kitu Fulani na sitaki kijirudie....

EPUKA kuongea maneno mengi pia EPUKA kuongea huku ukilia au sauti ikiwa inakwamakwama.


4) ONGEA UKWELI PALE INAPOBIDI  (UKWELI WAKO UJENGE KATIKA NAMNA FUPI ISIYO NA MAELEZO MENGI)

Kama MTU anazungumza nawewe hata kama ni bosi wako ikiwa anazungumza nawewe kwa ukali au kwa lugha chafu mwambie ukweli 

Mfano 

Akiwa anaongea kwa lugha chafu mwambie "siwezi kukusikiliza ukiwa na hasira, tutaongea muda mwingine"

Au....ikiwa MTU anaongea kwa ukali na kukufedhehesha hadharani mwambie "naomba tuheshimiane, siwezi kuvumilia uziumize hisia zangu.


5) JIHESHIMU SANA NA KUJITHAMINI KULIKO MTU YEYOTE

Kujiheshimu na kujithamini ni PAMOJA na kuvaa vizuri, kula vizuri, kuacha kutafuta MTU wa kukusifia Ili ujione mwenye furaha, kuacha kuongea vitu kwa lengo la kuchekesha au kutafuta huruma ya watu.


6) USITANGULIZE PESA MBELE SANA 

Usiruhusu pesa itawale maisha yako bali wewe ndo unatakiwa uitawale pesa.

Wewe ndio utaamua ni kipi ukifanye na kipi usifanye na usikubali MTU akutumikishe kisa pesa

Ukiwa MTU wa kutanguliza pesa MBELE watu watakuvunjia heshima sana kwa kuona wewe ni mrahisi inapokuja suala la pesa.


7) LAZIMA UJUE JINSI YA KUTUNZA SIRI ZA WATU

Kuropoka ya watu kwa watu wengine kunavunja heshima kwa kiasi kikubwa sana hivyo watakiwa KUWA mwaminifu ifikapo kwenye suala la KUTUNZA SIRI ZA WATU.


Pia waweza tazama video zetu mbalimbali YouTube kwa kubonyeza hapa chini👇👇👇👇👇👇






Post a Comment

0 Comments