Advertisement

MILIKI2

KUZA NYWELE ZAKO KWA WIKI MOJA TU.

 Mvuto wa nywele kwa mwanamke hutokea pale zinapochanwa au zinapobanwa katika mitindo tofauti



Leo tutaangalia namna ya kurefusha nywele na kuzijaza kwa KUTUMIA parachichi yai na asali.

Kabla ya kuanza kutengeneza mchanganyiko wetu, zijue faida za parachichi katika nywele;

1) Husaidia nywele kuwa nyevu nyevu wakati wote pia zenye muonekano mzuri, pia hazina ugumu wakati wa kuchana.

2) kulingana na potassium na Amino acids zilizo katika parachichi huzifanya nywele kukua kwa haraka sana 

3) Mmba kichwani husababishwa na NGOZI kukosa mafuta kwa hivyo parachichi Ina mafuta mengi ambayo yanafanya kazi ya kuzuia Mmba kwenye nywele zako

4) Kama nywele zako zimekatika na zimenywea parachichi inasaidia kuzipa uhai na muonekano mzuri zaidi

NAMNA YA KUTENGENEZA MCHANGANYIKO WETU

Chukua parachichi lililoiva katakata vipande vidogo vidogo Kisha chukua yai vunja na utoe kiini tu.....Kisha changanya kiini na vipande vya parachichi .......

Kisha chukua asali weka katika mchanganyiko wa parachichi na kiini Cha yai koroga mpaka viwe rojorojo

MATUMIZI 

Osha nywele zako kwa MAJI ya uvuguvugu Kisha zikaushe kwa taulo au kanga ....chukua mchanganyiko wako kata MISTARI na uwe unapaka katika MISTARI.... hakikisha nywele zote zimekolea.....vaa kofia ya plastic Ili nywele zipate unyevunyevu

Kaa dakika 20-30 Kisha osha nywele zako 

Fanya hivyo kwa muda wa wiki moja Hadi mbili na utaweza kuona matokeo mazuri yatakayokuridhisha 

Pia waweza tazama




Post a Comment

0 Comments