Advertisement

MILIKI2

KUZA NYWELE ZAKO KWA MAJI YA MCHELE



 Maji ya mchele yana vitamins B, C, E na amino acids ambavyo hivyo vyote vina faida nyingi kwa nywele kukua vizuri na kuwa zenye afya mfano, kurefusha nywele, kuzifanya nywele kuwa imara zisikatike ovyo, nywele kung'aa, kuzuia mba kwenye ngozi ya kichwa na kuzifanya nywele zisipoteze rangi yake ya asili.



Unaweza kuona umuhimu wa maji ya mchele ktk kukuza nywele zako, na kitu kizuri maji ya mchele unatengeneza mwenyewe kiurahisi bila gharama yoyote. Haya maji ya mchele unakuwa unaya tumia kama conditioner au hair spray kwa nywele.

Chukua mchele kikombe kimoja uchambue na kuuosha vizuri, kisha uweke mchele kwenye bakuli na tia maji vikombe 2, loweka kwa masaa 24, kisha chuja mchele na maji yake weka kwenye spray bottle na ongeza mafuta ya nazi au olive oil kiasi cha kijiko 1 cha chakula, funga spray bottle yako na maji ya mchele yatakuwa tayari kutumika kwa nywele zako.

Jinsi ya kuyatumia, maji ya mchele unaweza kuweka kila siku asubuhi au jioni ktk nywele zako au walau mara moja kwa wiki. Unakata mistari ktk nywele kisha unaweka maji ya mchele kwenye ngozi ya kichwa, na una spary maji ya mchele ktk ncha za nywele kisha taratibu una massage kichwa chako na nywele zako kuhakikisha maji ya mchele yameenea kichwa kizima na ktk nywele zote.

Hapa sasa nisikilize vizuri kama unatumia maji ya mchele kila siku au mara kwa mara, ukisha maliza kuweka maji ya mchele unaweza ukaendelea kuchana nywele zako na kupaka mafuta. Ila kama unaweka kwa wiki mara moja tu, kwanza osha nywele zako na shampoo, kisha weka maji ya mchele, halafu vaa kofia ya nywele ile ya plastic kwa dk 60 ila kufanya maji ya mchele yaingie vizuri ktk ngozi ya kichwa, mizizi ya nywele na ktk nywele zenyewe baada hapo huna haja ya kuosha nywele unaweza ukaendelea kutengeneza nywele zako unavyotaka, iwe kuset, kusuka  nk.

Maji ya mchele mimi huwa nayatumia kwa hata kwa wiki 2 sijaona yana haribika wala kutoa harufu, wengine huwa wana hifadhi ktk fridge, wengine huwa baada ya kutengeneza wana changanya na rose water, wengine huwa wamaloweka pamoja na maua ya yasmini ili kufanya maji ya mchele yanukie, wengine wanaloweka na vitunguu saumu vilivyo sagwa ili kuongeza virutubisho. Kifupi maji ya mchele ni mazuri na yana faida nyingi.

Post a Comment

0 Comments