Advertisement

MILIKI2

JE NAWEZA KUWA NA NGOZI NZURI YENYE AFYA?

 Jiamini NGOZI yako ni Nzuri sana.....unatakiwa kufata mambo haya machache Ili kuifanya ionekane Nzuri zaidi na yenye AFYA.


Ni ndoto ya WANAWAKE wengi KUWA na NGOZI safi, Nzuri na yenye AFYA......ndoto yako itatimia endapo utafata mambo haya


1) EPUKA KUSHIKASHIKA USO WAKO MUDA WOTE

Mikono hubeba bacteria hivyo ni rahisi kuhamishia bacteria hao katika NGOZI yako ya USO, na madhara kuanzia hapo kama vile kupata chunusi zisizoisha


2) USILALE UKIWA UMEPAKA MAKEUP

Inashauriwa na daktari wa NGOZI kwamba MTU YEYOTE hatakiwi kulala akiwa amepaka makeup......unapolala na makeup unaifanya NGOZI yako kushindwa kupumua hivyo hutengeneza uzio ambao ndio chanzo Cha kuharibu NGOZI yako 


3) PATA MUDA MZURI WA KULALA

Jitahidi ulale baina ya masaa 6-8, HII inasaidia kulinda NGOZI yako na kuifanya ijitengeneze vizuri KUWA yenye AFYA 


4) ZINGATIA VYAKULA VYA VIRUTUBISHO

Kula Vyakula vyenye virutubisho kama vile matunda, mbogamboga kwa wingi na Vyakula VYA baharini


5) EPUKA KUTUMIA VIPODOZI FAKE NA VILIVYOPITA MUDA WAKE

Vipodozi fake ndani yake hujazwa viambata sumu ambavyo kwa asilimia kubwa huharibu NGOZI yako....pia unatakiwa kuzingatia aina ya NGOZI yako unapochagua vipodozi (muda wa MATUMIZI ni muhimu zaidi kuuzingatia)


6) ZINGATIA KUNYWA MAJI KWA WINGI

MAJI ni uhai hivyo yatumie vizuri katika kuimarisha NGOZI yako....hakikisha kwa siku walau unakunywa glass zisizopungua 8


7) EPUKA KUKAA JUANI MUDA MWINGI

Jua Kali huharibu ngozi hivyo ni muhimu KUTUMIA viziba jua mfano kofia, miwani Ili kuikinga ngozi yako na miale hatari ya jua

Muonekano wako ni Ngozi yako.


Post a Comment

0 Comments