Advertisement

MILIKI2

JE UNATAKA TUMBO FLAT NA KUONDOA NYAMA UZEMBE ?

 KITUNGUU MAJI NA LIMAO KATIKA HATUA YA KUCHOMA MAFUTA TUMBONI.




Tunasonga mbele katika kupambana na kuchoma mafuta ya tumboni kwakutumia njia zetu za asilia kabisa na ukiwa nyumbani kwako.


Leo nawaletea juice ya kitunguu maji na limao katika safari hii yakukata kitambi.


        NAMNA YAKUANDAA HUU MCHANGANYIKO.


1:andaa kitunguu maji nusu yaani kipande kimoja

2:andaa kipande cha limao yaani nusu

3:andaa unga wa tangawizi kijiko kidogo cha chai.

4:andaa asali kijiko kimoja usitie nyingi sana au ukipenda usitie kabisa sii lazima hii ni kwaajili ya ladha tu.

5:andaa maji robo lita.


Kata kata kitunguu  maji pamoja na limao kata pamoja na maganda yake kisha tia kwenye brenda ongezea na maji ulio andaa robo lita kisha usage ili kupata mchanganyiko wako.

Usisage saana  baada yahapo chuja hayo makapi yake ili kupata hiyo juice yake kisha tia kijiko kidogo cha tangawizi ya unga ongeza na asali kijiko kimoja cha chai baada ya hapo koroga ichanganyikane kisha uache kwa dakika 5 ili mchanganyiko wako ukoleane kisha baada ya hapo unaweza ku enjoy mchanganyiko wako.


        MATUMIZI 

Tumia mchanganyiko huu kutwa mara 2 Asubuhi na jioni pia unaweza kuandaa ya kutwa nzima ili utumie kutwa mara 2.


Kwakukazania mchanganyiko huu na ukiwa umefanikiwa kupunguza kiwango cha wanga mwilini pamoja na matumizi ya vinywaji vya sukari mwilini hapo utaona matokeo mazuri kwa haraka sana.


Post a Comment

0 Comments