Advertisement

MILIKI2

LAINISHA USO KWA NYANYA NA ASALI (BABY FACE)

 

LAINISHA USO KWA NYANYA NA ASALI


Watu wengi wanadhani kutumia vipodozi vya asili ni urembo wenye mchakato mrefu na mgumu lakini kama unaipenda ngozi yako naamini hautaona ugumu wa kuitunza kwa vipodozi vya asili. Ifuatayo ni namna ya kulainisha uso wako kwa nyanya na asali, utaonekana ni mwenye Baby face na MVUTO wa ajabu


Chukua nyanya moja kubwa iliyoiva kisha imenye na kuisaga hadi iwe uji na kisha changanya asali na uji wako wa nyanya mpaka vichanganyike vizuri, baada ya hapo paka mchanganyiko wako usoni na  acha kwa robo saa hadi ukauke kisha nenda kaoge.


Kisha kausha uso vizuri na taulo safi na rudia hivyo mara mbili kwa wiki na utapata matokeo mazuri kwa ngozi ya uso wako.
Pia Kwa wale wenye chunusi njia hii inawafaa zaidi Kwa matokeo Bora.
Pia waweza tazama mitindo tofauti ya kuwasuka watoto👇👇👇





Post a Comment

0 Comments